Man Fizo Mkali wa Filamu ya ‘Nimekosea Wapi’
Nimekosea Wapi kutoka Steps Entertainment ni moja kati ya filamu zenye ubora wa juu zaidi kati ya filamu kadhaa zilizoingia sokoni mwaka huu.
Mbali ya kuwepo na mastaa kadhaa kama Gabo Zigamba kwenye filamu hiyo yupo Salum Saleh ‘ Man Fizo’ ndiyo mtengenezaji na amecheza kwenye filamu hiyo.
Wadau wengi waliotazama filamu hiyo wamemtabilia kufanya makubwa zaidi kwenye tasnia ya filamu hapa bongo.
Kama nawewe umeitazama ‘Nimekosea Wapi’ , funguka umeonanini kwa Man Fizo.