Wema Sepetu Adai Mwaka 2006 Ulikuwa Mwisho wa Miss Tanzania
staa wa bongo movie, Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 amesema hajui lolote kuhusu mashindano hayo zaidi ya kuwa mwaka alioshinda yeye ndiyo ulikuwa wa mwisho kwa mashindano hayo.
Mwaka jana mashindano ya Miss Tanzania yalifungiwa na BASATA kutokana na tuhuma za upangaji wa matokeo uliosababisha kupoteza msisimko na mvuto wa mashindano hayo. Hata hivyo mashindano hayo yamerejea tena.
Akiongea na Times FM, Wema alisema, “Sijui ni nini hasa kimetokea, maana mimi sifuatilii kabisa Miss Tanzania kwa sasa wala sijui Miss Tanzania mwaka huu anaitwa nani, nimeamua kuachana nayo kabisa sijui lolote, ila ninachojua mimi 2006 ndio mwaka wa mwisho wa Miss Tanzania.”
Bongo5