Rais Amefanya Mabadiliko Baraza la Mawaziri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri huku akimteua Mbunge wa Buchosha Dk. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri walioteuliwa katika mabadiliko hayo wataapishwa Jumatatu asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwananchi