-->

Mwimbaji wa Injili, Goodluck Gozbert Afunguka Kuhusu Mashairi Yake Maisha Yake

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert ameeleza kwamba mashairi ya nyimbo zake huwa yanaeleza maisha yake. Akizungumza katika kipindi cha Clouds360, mwimbaji huyo ameeleza kwamba yeye alizaliwa katika familia masikini na kulelewa katika mazingira magumu sana baada ya baba yake kufariki.

Goodluck Gozbert

Goodluck Gozbert

Mtunzi huyo wa kibao maarufu cha ‘Acha Waambiane’ amezindua wimbo mpya unaoitwa ‘Ipo Siku’ ambao kwa mara ya kwanza kabisa umeonekana kupitia Clouds360 ya Clouds Tv. Video hiyo imetengenezwa na mkongwe wa Video Bongo , Adamu Juma na kama kawaida ya Goodluck Gozbert mashairi ya ‘Ipo Siku’ yamejaa ‘inspiration’.

Goodluck Gozbert amefichua kwamba yeye ndio ‘producer Lolipop’ aliyetengeneza wimbo wa Ben Paul unaotamba kwenye redio mbalimbali kwa sasa; ‘Moyo Mashine’ na nyimbo nyingine kali za Bongo fleva. (Anaproduce Bongofleva wakati yeye anaendelea kumtukuza Mungu kwa nyimbo za Injili ).

Cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364