Hemed PHD Afunguka Madhara ya Kutoka na Staa
MUUZA sura kwenye filamu za Kibongo, Hemed Suleiman ‘Hemed PHD’ amefunguka kuwa japo ni staa na mtu maarufu Tanzania lakini hata siku moja hajawahi kufikiri kuwa atakuja kujihusisha kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa kike kutoka Bongo kwa sababu anafahamu madhara yake.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, PHD aliongeza kuwa madhara ya kutoka na staa kimapenzi husababisha vyombo vya habari kuwamulika wahusika muda wote jambo ambalo yeye halipendi ukizingatia anafuata misingi ya dini yake ya Kiislamu inayomfanya aamini kuwa uhusiano ni suala binafsi ambalo halihitaji kushereheswa na watu.
“Unajua vyombo vya habari vinapofahamu kuwa unatoka na staa fulani vinaanza kukuandama wewe pamoja na huyo mpenzi wako. Si kitu kizuri kwa sababu mnapotofautiana pia vinaanza kuwazungumzia jambo ambalo wakati mwingine linaweza kusababisha hata msirudiane kutokana na misteki tu ndogo. So mimi sipendi kabisa maisha yangu yamulikwe ndiyo maana nimejiweka kando kwenye suala zima la uhusiano kutoka na staa,” alisema PHD.
Chanzo:GPL
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA