Johari Afungukia Ishu ya Kuolewa Mke wa Pili
Muigizaji wa filamu nchini Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka na kuweka wazi sababu yeye kubadili dini na kuwa muislam na kudai kwamba mwanaume hajawa sababu yeye kubadili dini bali yeye mwenyewe ana damu ya uislam ndani yake kwani wazazi wake mmoja ni mkristo na mwingine ni muislam.
Johari kupitia kipindi cha eNEWS alisema hana mpango wa kuolewa mke wa pili na wala hilo suala haliwezi kutokea kwake kwani anahitaji kuwa na mume mmoja tu na hawezi kuwa na amani kuona anaingia sehemu ambayo kuna mwanamke kama yeye.
“Kwa kweli mimi sina mpango wa kuolewa mke wa pili na sitoweza kuolewa mke wa pili, Kwanini labda niolewe mke wa pili ? Mimi nahitaji kuolewa ndoa moja na niwe na na mume mmoja na kuishi naye, siwezi kuingia sehemu ambayo mwanamke mwenzangu ameshakaa kwa hiyo kama kuna sehemu mtu ameshaoa hiyo sehemu siwezi kuingia hicho ndicho nachoweza kukwambia” alisema Johari.
Mbali na hilo Johari aliwataka wasanii wa kike wanaochipukia kwenye uigizaji kuingia kwenye makundi mbalimbali kwani huko wanaweza kujifunza mambo mengi ambayo yataweza kuwasaidia kufikia malengo yao kwenye uigizaji, kuliko kutegemea ukaribu na mtu fulani au kutumia miili yao kwa baadhi ya wasanii wa kike kwani anasema hawataweza kufikia malengo yao.
“Nawashauri wasanii wanaochipukia kujiunga na makundi mbalimbali kwani kule wanajifunza mambo mengi, ndiyo maana leo hii ukiwaangalia wasanii ambao tumepitia kwenye makundi tupo tofauti sana na wale ambao hawajapita kwenye makundi ya sanaa, nawaambia wasanii wa kike kutegemea kufanya kazi kwa sababu unajuana na mtu fulani, au kutumia mwili wake sawa wanaweza kweli kufanya lakini hawatafikia malengo yao hivyo ni bora wajifunze na kuvumilia kwenye makundi mbalimbali ili wajijenge zaidi kwenye sanaa” alisema Johari
eatv.tv