Mama Afunguka Wema Kurudiana na Diamond!
Licha ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuibuka na kukanusha sakata lao la kurudiana, bado madai ya wawili hao kutoka kwa siri yamekuwa yakishika kasi kiasi cha kumfanya mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu naye kulazimika kufungukia taarifa hizo.
MADAI YA KURUDIANA
Watu walio karibu na mastaa hao wanadai kuwa, siyo siri, Wema na Diamond wanakutana wanapohitajiana ila ni vigumu kukiri kwa kuwa kila mmoja ana mtu wake.
Watoa ubuyu hao walizidi kufunguka kuwa, isingekuwa rahisi watu kuvumisha kitu ambacho hakipo na kitendo cha mitandao mingi ya kijamii kulianika hilo kinaashiria kuwa kuna jambo nyuma ya pazia.
“Wema ameibuka na kusema hajarudiana na Diamond ila wanashirikiana katika kazi tu, sasa sisi tunawaona wakijivinjari kwa siri na usitarajie kwamba yupo atakayekiri maana Wema yuko na Idris (Sultan) na Diamond yupo na Zari…
“Lakini pia mitandao mingi ya kijamii inaandika huku wakiweka viashiria vya kurudiana kwao, sasa kama wao wanabisha, wabishe tu lakini sisi ndiyo tunaujua ukweli na ipo siku wataumbuka,” alisema mtu wa karibu wa Wema ambaye anadai alimshuhudia Diamond kwa macho yake akiingia chumbani kwa Wema.
UZALENDO WAMSHINDA MAMA WEMA
Kufuatia maneno kuzidi kuenea mithili ya moto wa kifuu kuhusu Wema na Diamond kurudiana kwa siri, Ijumaa lilizungumza na mama Wema aliyewahi kuonesha dhahiri kutotaka mwanaye kuwa na Mbongo-Fleva huyo na kwa mara ya kwanza alifunguka kilichomo moyoni mwake.
Mama huyo ambaye umri umekwenda lakini bado anaonekana ‘yumo’ alisema kuwa, haamini hayo yanayosemwa na watu kwamba Wema karudi kwa Diamond kwa kuwa ingekuwa hivyo yeye angekuwa ameshagundua.
“Kwanza niseme tu kwamba, sidhani na wala sitarajii mwanangu kurudiana na Diamond. Ni kitu ambacho hakiwezi kutokea, ninachoona hapo ni mambo ya uzushi ya kwenye mitandao.
“Ninachojua mimi, Wema yuko kwenye ulimwengu mwingine wa kimapenzi, arudi kwa Diamond kwa kipi? Ana maisha yake mengine anayoyafurahia na hivyo kusema kamrudia Diamond hainiingia akilini.
“Najua wengi walidhani hivyo baada ya Wema kuposti kitu f’lani kumhusu Diamond kwenye mtandao lakini najua alifanya vile ili kuwakata vilimilimi waliokuwa wakimtukana na kudhani ana bifu na Nasibu,” alisema mama huyo.
AMPEKENYUA MAMA DIAMOND
Licha ya kwamba ni muda mrefu mama huyo hajawahi kumzungumzia mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ tangu wakati ule alipokuwa akimponda Diamond kuwa hata kwa dawa hawezi kumuoa binti yake, safari hii amempekenyua kwa kudai kuwa hamjui na hata akikutana naye hawezi kumtambua.
Mama Wema alisema hayo baada ya kupewa madai kwamba, anajifanya hajui kuwa mwanaye amerudiana na Diamond wakati hivi karibuni walionekana pamoja nyumbani kwa mama Wema maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
“Niseme tu kwamba mama Diamond simjui, hata leo nikikutana naye siwezi kumtambua labda anishtue, ila nimpongeze tu kwa uzalendo aliouonesha hivi karibuni wa kumposti Wema akiwa na Idris kwenye ile shoo ya Black Tie na kuandika maneno yaliyoonesha uzalendo,” alisema mama Wema.
Chanzo:GPL