Waziri Nape Azindua Filamu ya Sikitu!
Waziri Nape Nnauye akiongea jambo kabla ya kuizindua filamu ya Sikitu, ndani ya ukumbi wa sinema uliopo ndani ya Jengo la Quality Center jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa filamu hiyo, Kajala Masanja (wa pili kutoka kulia), akiingia ukumbini hapo tayari kwa kushuhudia zoezi la uzinduzi huo.
Nape katikati, akifuatilia filamu hiyo muda mfupi baada ya kufanikisha uzinduzi rasmi.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi katikati na Queen Darleen kulia wakitazama filamu hiyo.
Msanii wa filamu Yusuf Mlela akifuatilia filamu hiyo.
Baadhi ya warembo wakiwa kwenye pozi muda mfupi baada ya kumaliza kuishuhudia filamu hiyo.
Muigizaji wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, (kushoto), akiwa katika pozi na msanii Linex .
Wazira wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye usiku wa kuamkia jana alikuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Filamu ya Sikitu, na kupewa heshima ya kuizindua filamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Sinema uliopo ndani ya jengo la Quality Centter Barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam, ambapo filamu hiyo iliandaliwa na msanii wa tasnia hiyo Kajala Masanja.
Akizungumza kwenye Uzinduzi huo, Nape alisema kuwa filamu ya Sikitu, ina ubora unaohitajika kuendelezwa na waandaaji wengine wa filamu hapa nchini, ili ziweze kupata nafasi kubwa zaidi za kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema kama ilivyofanyika kwa filamu hiyo.
Pia Nape aliagiza kuwa kuanzia leo mtu yoyote atakaye atakamatwa na filamu au kazi ya msanii yoyote hapa nchini na nje ya nchi ikawa haina stakabadhi ya TRA, basi achukuliwe hatua kama wahalifu wengine wa makosa ya uharamia.
“Serikali tumejipanga kusimamia kazi za wasanii kwa ukamilifu, hivyo kuonyesha tumejipanga tutakuwa na operation za mara kwa mara kwa ajili ya kukamata wale wote wanaohujumu kazi za sanaa yetu na lengo ni kuboresha na kuwafanya wasanii wa nchi hii wanufaike na kile wanachokifanya kutokana na sanaa ya kazi zao,” alisema Nape.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.