-->

Mzee Chilo Awashukia Wasanii Kuhusu Kunyonywa na Wadosi

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Chilo amesema siyo kweli kwamba wasambazaji Wakiindi wanawanyonya wasanii wa filamu.

Mzee Chilo

Mzee Chilo

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Mzee Chilo amesema kuwa wasanii wengi kwa sasa wanafanya filamu mbovu ndio maana filamu zao zinakosa soko kwa Waindi.

“Wanaosema kwamba bongo movie imeshuka sijui hizi taarifa wanazipata wapi, mimi nipo kwa miaka mingi na wasambazaji wakiindi na sijawai kupata tatizo lolote kusema kweli,” alisema Chilo. “Mimi nadhani wanaosema Waindi wanaaribu soko la filamu siyo kweli, huo ni uongo, wao ndio wanafanya filamu mbovu ndio maana hazifanyi vizuri,”

Muigizaji huyo amewataka wasanii wa filamu kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364