-->

Kupanda na Kushuka kwa Shirikisho la Filamu

SHIRIKISHO la filamu Tanzania (TAFF) lipo kwa miaka kadhaa huku tukishuhudia changamoto nyingi zinazokabiri shirikisho hilo ambalo pamoja na kuanzishwa kwake ni chombo kisichotengeneza fedha kutokana na vyama vinavyounda TAFF kukosa miradi kama michango kutoka kwa wanachama wake.

Mwakifwamba

Rais wa Taff Mwakifwamba

Taff imekuwepo kitambo lakini imekuwa Lulu baada ya kuanzisha michakato yenye tija kwa wasanii na wadau husika kwa chombo hicho kilicho chini ya Rais wake Simon Mwakifwamba ambaye amefanya mengi akishirikiana na Hiluka Bishop Deosonga Njerekela na bodi ya TAFF.

Wengi wanabenza kuwa uwepo wa Rais huyo hakuna kitu lakini ukweli ni kwamba Mwakifwamba ni mwanaharakati ambaye amejitoa kwa asilimia kubwa kujenga tasnia ya Filamu Swahilihood akijaribu kujenga mahusiano mema kati ya wasanii na wasanii.

Taff wana vitu vya kujivunia kwa wasanii ambavyo ni pamoja na kutambulika kwa Serikali na jamii kwa ujumla hata kuweza kurasimishwa kwa tasnia ya Filamu na kuwa kitu rasmi kwa wasanii na wadau wa filamu wamewaunganisha wasanii wa mikoani na nchi nzima .

Taff imeanzisha mfuko wa Wasanii ambao unajulikana kama TAFF TRUST FUND mfuko ambao unasimamiwa na wajumbe wa kutoka sehemu mbalimbali kama vile Masoud Ali ‘Masoud Kipanya’, Jack Gothan, Prof. Ambandina Lyamba Asha Mtwangi na Sauda samba ni watu wenye nafasi zao katika jamii.

Mfuko huu ukitunishwa ni wazi kuwa miradi iliyofanyiwa utafiti inaweza kuwezeshwa na TAFF na kutoa mchango mkubwa kwa wadau wa filamu kwani kuna uwezekano watengenezaji wa Filamu wakatumia mfuko huo kwa kukopa na kutayarisha kazi zao baada ya kukosa dhamana katika mabenki.

Taff ina kampuni iliyosajiliwa ya TAFF CREATIVE LTD kampuni hiyo ni mahsusi hasa katika kuhakikisha ubora wa kazi za filamu sambamba na uzalishaji wa sinema kwa ajili ya kwenda sokoni, ni chombo muhimu sana kulingana na hali ya soko ilivyo kwa sasa.

Na kwa habari za uhakika tayari kampuni hiyo ipo katika maongezi na taasisi za kibenki kwa ajili ya kupatiwa mtaji zaidi ya Dola milioni tatu katika hatua za awali katika ujenzi wa miundo mbinu ikiwa tayari wakiwa na eneo kwa ajili ya mji wa Filamu huko Bagamoyo.

Kupitia TAFF kuna wasanii wanaweza kulipiwa Bima ya Afya kwa wale wazee wasio na uwezo jambo ambalo ni muhimu sana tukishuhudia kuwa mara kadhaa wasanii wamekuwa wakikumbwa na matatizo mbalimbali huku hata misiba ikitokea huhitaji msaada wa mazishi.

TAFF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa mwaka huu walifanya makubwa kwa kuwezesha kuandaa tuzo kubwa zilizojulikana kwa TAFA Tanzania Film Awards na kufanyika katika ukumbi wa kisasa kabisa wa Mwalimu Nyerere huko Posta, ikiwa ni moja kati ya ukuzaji wa Tasnia ya Filamu.

Lakini jambo kubwa kuliko yote ni la kutumia fedha nyingi katika kufanya utafiti na kuandaa sera ya filamu ambayo hakuna katika nchi yetu wengi tunaamini kuwa Sera ya Filamu ikiwepo itakuwa ni mkombozi wa wadau wa tasnia ya Filamu na kusonga mbele.

Pamoja na kuwa na mashirikisho manne lakini bado utaona TAFF imekuwa ni shirikisho lenye nguvu na kufanya ushawishi kwa watawala na wabunge katika kuhakikisha tasnia ya filamu inatambulika na kuwa ni taasisi yenye uwezo wa utengenezaji wa ajira kwa watu wengi.

Hatua inakwenda kwa kasi sana ni imani yetu kuwa baada ya uchaguzi wa vyama vyake na kupata viongozi wa mikoa na Taifa kasi hiyo itaendelea na kupiga hatua katika tasnia ya filamu ombi letu kama FC ni kujenga misingi imara katika kuhakikisha lengo linafikia.

Ni imani yetu kuwa uwepo wa Rais Simon Mwakifwamba, Makamu rais Deosonga Njerekela, Katibu Bicco Mathew, Paul Mtendah, John Kallage, Myamba na wajumbe wote wa Bodi wanaweza kutuvusha hapa na kwenda sehemu nyingine msingi upendo Weledi vitangulie .

Changamoto kubwa kwa Taff ni imarishaji wa vyama vyake lakini kuwaweka pamoja wasanii wote jambo ambalo Mwakifwamba analifanya ikiwa ni pamoja kukutana na kundi la wasanii nyota la Bongo movie na matokeo chanya kwani wapo katika makubaliano ya kuwa pamoja.

Taff imepiga sana kwa kuhakikisha inajenga misingi imara kwa wasanii na kuwaweka pamoja huku ikiwa na mipango mikubwa ikiwa imeazimia kuweka vitega uchumi lukuki kwa ajili ya wasanii na wadau wa filamu.

Chanzo: FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364