Mr.Blue: Mboga 7 Imenipa Heshima Kwenye Hip hop
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Herry Sameer ‘Mr Blue’ anayetesa kwa sasa na wimbo wake wa Mboga Saba aliomshirikisha nguli mwingine kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva Ali Kiba, amefunguka na kuelezea hisia zake za moyoni kuhusu wimbo wake huo ulio kwenye mtindo wa Hip hop.
Mr Blue kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ujumbe ufuatao, “Nyimbo yangu ya Mboga 7 imekuwa nyimbo yangu ya kwanza ya rap/hip hop kutimiza watazamaji milioni moja kwenye mtandao wa YouTube ndani ya hii miaka miwili. Achana na hizi za kuimba nazungumzia Hip hop.” Alisisitiza mwanamuziki huyo.