Jux Afungukia Muonekano Wake na Muziki
Msanii Jux ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Wivu’ amefunguka na kusema muonekano wake pamoja na mavazi yake yamemsaidia kumuweka mahali fulani katika kazi yake ya muziki.
Jux alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa alitambua kuwa muonekano unaweza kumsaidia katika muziki ndiyo maana kabla ya kutoka kwenye muziki alianza kulifanyia kazi jambo hilo ambalo leo hii limezaa matunda kwenye muziki wake.
“Unajua mimi kabla ya kutoka nilikuwa natambua kuwa muonekano wa msanii unamsaidia mtu kufikia sehemu fulani, kwani ukiwa msanii lazima ujiweke tofauti na watu wengine wa kawaida, hivyo nilifanyia kazi hilo kabla sijatoka kimuziki, mpaka sasa nilipofikia kwenye muziki wangu naweza kusema muonekano pamoja na aina ya mavazi nayokuwa navaa yamechangia kama asilimia arobaini” alisema Jux