Kajala: Nataka Kuzaa Mtoto wa Kiume
“Nahitaji kuzaa mtoto wa kiume ili Pamela naye ajivunie kuwa na kaka, siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti, tayari ninaye wa kike sasa ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume.” Ni kauli ya Kajala Masanja mwanadada anayefanya vyema kwenye soko la filamu nchini.
Kauli hiyo ya Kajala imekuja siku chache baada ya kuulizwa na Global Digital kama ana ndoto za kupata mtoto mwingine siku za hivi karibuni wakati mumewe akiwa bado yupo gerezani.
Mwanadada huyo alifunguka zaidi na kusema, “Hakuna mwanamke asiyependa kuwa na mtoto wa kiume japokuwa mtoto ni mtoto, na nipo tayari kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia gharama za matunzo ya mtoto kwa kushirikiana.” Alisisitiza.
Chanzo:GPL