-->

Diamond Platnumz Awavuruga Mashabiki

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ maarufu kama Simba ameachia kipande kidogo cha wimbo ambao ni remix ya ‘All The Way Up’ ambayo na yeye ameshiriki na kuchana katika wimbo huo.

diamond9022

Diamond Platnumz

Mashabiki wengi wa Diamond Platnumz wamefurahishwa na jinsi msanii huyo alivyoweza kuchana vyema huku maneno yake ya kiswahili aliyoyatumia katika ngoma hiyo kuonesha kuwakosha wengi na kuwavuruga kabisa kwa furaha kutokana na midondoko yake kwenye ‘remix’ hiyo ambayo haijafahamika bado ataiachia lini.

“Moja ya mistari ya Diamond kwenye wimbo huo ni pamoja na “Hasa waambie dada zao Kariakoo waje Ulaya, wanajenga majungu mimi najenga vibanda, wanatisha visu kumbe mimi nina panga, mimi namuomba Mungu wanakesha kuwanga” Amesikika Diamond Platnumz akiimba

Baada ya kupost kipande hicho cha wimbo huo haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki zake ambao wameonesha kufurahishwa na kipande cha ‘remix’ hiyo

“Diamond sasa jamani ananifanya nitetemeke mwili mzima anafanya vitu vya ajabu sana. Waambie na dada zenu waje Ulaya ha ha ha ha wamesikia” Shaibu Mgwaluv

Diamind3

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364