-->

Aunty Ezekiel Afunguka Kuhusu Mipango ya Ndoa

Nyota wa Bongo Movie Aunty Ezekiel amesema hayuko tayari kuolewa kwa sasa, na kwamba bado hajafikiria kuolewa kwa kuwa suala la ndoa linahitaji maandalizi ambayo dbado hajayafanya kwa sasa.

aunty78

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo

Miongoni mwa story ambazo zilibeba headline juma lililopita, ni pamoja na issue ya mwana tasnia ya filamu nchini, Shamsa Ford kuolewa na mjasiriamali Rashid maarufu kwa jina la Chidmapenzi,

eNewz ilibidi ijiridhishe na ilifanikiwa kumpata muigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel ambaye alikuwa mpenzi wa zamani Chiddi na kutaka kufahamu ndoa yake na Moses Iyobo itafanyika lini.

Mbele ya camera za eNewz, Aunty Ezekieli alifunguka kuwa ndoa sio maigizo bali ni kitu kigumu na kinatakiwa kujiandaa vyema na kwamba siyo kwakuwa Shamsa kaolewa basi na yeye akimbilie kuolewa.

“Ndoa sio kitu cha mchezo, ndoa sio maigizo. Kwahiyo sio kwasababu Shamsa kaolewa na mimi niseme kesho tegemeen, ndoa ni kitu ambacho mtu anatakiwa ajipange, naamani Shamsa kafanya hivyo namimi ikifika muda nitawaza, bado sijafikiria” Alisema Aunty Ezekiel.

Hatahivyo mbali na suala la ndoa, eNewz ilitaka kujua kuhusiana na mipangilio ya Aunty Ezekiel kwenye tasnia ya filamu baada ya kuonekana amepotea kwenye tasnia hiyo kwa madai kuwa baada ya kuwa kwenye mahusiano na Moses Iyobo ambaye amezaa naye mototo mmoja.

Aunty alikanusha kupotea kwenye game na matukio yote ya filamu bali ameweka wazi kuwa amekua kimaisha kutoka hatua moja hadi nyingine na kwamba ndiyo maana ameamua kuachana na mambo ya ujana na kutafuta kiki.

Aunty Ezekiel amesema “Aunty Yule ambaye nilikuwa nikitoka kwenye magazeti zamani kuwa nimetoka uchi, nimetoka na fulani siyo huyu. Kwasasa mimi ni mama na nimekua ndiyo maana hunioni nikifanya hayo na ndiyo maana watu wanasema nimepotea kwenye game”

“Wale ambao wanatembea uchi ninawaomba waache kwa kuwa hazitawasaidia, Unakuta mtu anatafuta kiki lakini jina lake halikui. Huu wakati nilioufikia siyo wa kutafuta kiki bali ni wa kufanya kazi” alimalizia Aunty Ezekiel kwa kutoa ushauri.

 eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364