Najma Afungukia Ishu ya Bayser na Baraka Da Prince
Baada ya Byser kutangaza kuchukua hatua za kisheria kwa Naj au Baraka endapo atagundua kuwa wao ndiyo walianzisha ile skendo iliyomuhusisha yeye kuwa anachepuka na Naj ili kuupa ‘kiki’ wimbo wao mpya, eNewz ilimtafuta Naj ili kusikia majibu yake.
Naj alisema “Sioni kama kuna tatizo, ila naona tu haya mambo yanakuzwa na maneno ya watu, Mimi huwa sifanyi kazi kwa ‘kiki’, na kwa sasa chochote nitakachokisema ninaweza nisieleweke hivyo nimeamua ni bora nikae kimya tu”.
Pia Mr. Blue a.k.a Byser alisema kuwa aliongea na Baraka na Baraka akasemea kuwa hajui uzushi huo umetokea wapi, hivyo wakayamaliza bila ya kuwa na tatizo.
Hata hivyo Byser alimaliza kwa mkwara akisema “Kama hawa watoto wadogo ni wao ndiyo wameanzisha hii skendo, nikigundua ni hivyo basi nitawachukulia hatua, na pia mimi siwezi kurudia matapishi yangu”.
eatv.tv