Banana Zorro Afungukia Singeli
Hakuna ubishi kuwa muziki wa Singeli umeteka vichwa vya mashabiki wengi kwa sasa nchini. Banana Zorro amefunguka juu ya matarajio ya kufanya muziki huo.
Muimbaji huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa ana uwezo wa kufanya muziki huo lakini kwa sasa hajafikiria kuufanya.
“Mimi nina uwezo wa kufanya kila muziki, lakini Singeli kwangu kwa sasa sijafikiria lakini naona ni muziki mzuri ambao unakuja vizuri, wasanii wake wakiutumia vema unaweza kutoka kimataifa na kuipaisha zaidi Tanzania,” amesema Banana.
Mpaka sasa wasanii wakongwe kama Profesa Jay na Rama Dee wameukubali muziki wa Singeli hadi kuwashirikisha nyota wa muziki huo kwenye nyimbo zao.
Bongo5