-->

Miss Tanzania Alia Kutelekezwa na Kamati

Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World’, ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza.

miss44

Miss Tanzania 2016 Diana Edward

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diana ambaye kwa sasa anatakiwa awe kwenye maandalizi ya mashindano ya Miss World, amesem abado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache  kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.

Amesema kuwa kwa sasa yeye anachohitaji kwa sasa ni suport pamoja na msaada mkubwa kutoka kwa serikali, kwani yeye binafsi anajitahidi kufanya pale anapoweza.

“Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve”, alisema Diana.

Kwa upande wa msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania ameruka kuhusika na suala hilo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364