Muhogo Mchungu Anatudai – Solid Ground Family
Kundi la muziki wa bongo fleva Solid Ground Family ambao wameanza kitambo kwenye game ya muziki na mpaka sasa wapo kwenye game, wamekiri kitendo cha kumdhulumu muigizaji mkongwe wa filamu Muhogo Mchungu.
Wakizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, wamesema deni hilo la Muhogo mchungu walilipata wakati wanaenda kufanya shooting ya video ya Bush Party’ ambayo ni ya kitambo sana, lakini hawakummalizia malipo yake mpaka sasa.
“Ni kweli Muhogo Mchungu anatudai, mpaka leo hatujampa, ile ilikuwa tumeenda Goba kufanya shooting ya ‘Bush Party’, tena kipindi hicho Goba hakuna nyumba kama ilivyo sasa, ilikuwa pori kabisa kama mlivyoona kwenye video, sasa tukakubaliana kumlipa sh. elfu 50, ila hatukumpa yote na mpaka sasa anatudai, huo ni ukweli wala siyo maneno ya watu”, alisema mmoja wa wanaounda kundi hilo.
Kundi hilo limesema wapo tayari kumalizana naye kama bado ana kinyongo nao, kwani wana imani mdeni wao kawasamehe kutokana na kuwa muda mrefu umeshapita tangu kazi hiyo ifanyike.