Idris Aingilia Bifu la Diamond, Dimpoz, Kiba
WAKATI gumzo la mvutano na kutupiana vijembe kwa wasanii watatu, Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na Ali Kiba likiendelea, mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan naye ametoa neno kuhusiana na hicho kinachoendelea.
Wasanii hao wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba‘King Kiba’ na Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz ’ wamekuwa wakionekana kuwa karibu siku za hivi karibuni na kutupiana vijembe na rafiki wao wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’, hali iliyofanya kuwa na mgawanyiko wa mashabiki wanaounga mkono kila upande.
Idris ambaye pia ni mchekeshaji na mtangazaji wa redio, amewachambua wasanii hao kitabia na kueleza kile ambacho kinaweza kuwafanya wapatane.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Idris alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond.
“Bifu la Diamond, King Kiba na Ommy Dimpoz ninachokijua inatokana na kila mtu kujiona kuwa ni bora zaidi ya mwenzake.
“Hilo ndilo tatizo kubwa ambalo limewafanya washindwe kuelewana na ndiyo maana wanaibua sinema kila kukicha. Hao wote ni jamaa zangu na ninafahamu vizuri tabia za kila mmoja wao.
TABIA ZA KIBA, DIAMOND, DIMPOZ
“Kiba ni mtu mwenye majigambo, siku zote anaamini kila anachokiweza yeye hakuna mwingine anayeweza kuwa juu, ikitokea amezidiwa basi ishu ya majigambo ndipo inapoanzia na kujikuta akikosana na wenzake.
“Dimpoz ni mtu mvivu sana, yaani huwa hapendi kujibidiisha katika maendeleo yake hadi asukumwe, hivyo tabia hii mimi naona kama ndiyo kisa kinachosababisha kushindwa kufanikisha mambo yake mengi na mwisho wa siku anajikuta akiishia kugombana na wenzake.
“Diamond namuona mchapakazi sana na anapenda maendeleo ya haraka kiasi kwamba akiona kama kuna mtu anataka kuremba mbele yake huwa hakawii kumpuuza huku akiendelea kufanya mambo yake.
“Ila Diamond naye ana vijitabia vya uswahili-uswahili hivi, mfano kupigapiga vijembe, hii inatokana
na mazingira aliyokulia.
“Kwa maelezo haya naamini unaweza kuelewa kwa nini watu hao ni vigumu kuwa kitu kimoja.
DIAMOND VS KIBA
“ Hivi unajua ugomvi wa Diamond na Kiba siku zote nimekuwa siuelewi , maana kila mmoja nikimuuliza kwa upande wake, hakuna aliyewahi kunithibitishia kuwa wanatatizo zaidi ya kutuhumia na juu ya kushindwa kushirikisha na kwenye moja ya kolabo yao.
DIAMOND VS DIMPOZ
“Watu wanatakiwa watambue kuwa hawa wanajuana vizuri, kila mmoja ana udhaifu wake, hakuna anayeweza kuwapatanisha labda wao wenyewe waamue kuelewana kivyao. Wala siamini kuwa Wema anahusika kwenye bifu lao.
“Wapo wanaodai kisa ni ile ishu ya Wema kufanya video na Dimpoz, mimi siafiki hilo, ingekuwa hivyo basi Diamond angekuwa ameshanipiga risasi kabisa kwa kuwa nilikuwa mpenzi wa Wema.
“Tumekuwa tukikutana na tunazungumza freshi tu, mimi na Diamond tunaheshimiana japo kwa sasa siyo rafiki yangu wa karibu na hata tulipokuwa tukikutana tulikuwa poa tu.
“Katika bifu hili la Diamond na Dimpoz ukichunguza kwa makini utagundua limeiva baada ya wote wawili kuachia nyimbo, hivyo kwa mwenye upeo ataona tu kuwa wana njia ya kupenyeza muziki wao kwa kutumia vijembe.
“Najua ipo siku Diamond na Dimpoz watakuja kupatana, waachwe tu, kwa sasa hata waitwe mashekhe na mapadri na uweke viongozi wa kuu wa nchi, kamwe hawawezi kuwaweka sawa.
“Bifu lao litakuja kutulia tu siku moja wao wawili watakapoamua, kwani hata tukizidi kupiga makelele sana hakuna hata mmoja anayeweza kusema ukweli.
“Kutokana na hali hiyo hakuna haja ya kupigizana kelele hapa, zaidi wanachotakiwa kukubali wasanii wenzangu ni kwamba, Diamond ni mchapa kazi na hapendi wenzake wasifanikiwe, hivyo tuendelee kusapotiana na kuiga uchapakazi huo,” anasema Idris.
Chanzo:GPL