Raymond Amshukuru Diamond Alichomfanyia Kwenye Video Mbili
Raymond ameendelea kumshukuru bosi wake wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz kwa kile anachomsaidia kupitia muziki wake.
Hitmaker huyo wa Natafuta Kiki, amefunguka kwa kuweka wazi kuwa nguo alizovaa kwenye video ya ‘Kwetu’ na ‘Mugacherere’ zilikuwa za bosi wake huyo.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray Vanny ameandika:
Kwenye Video ya #KWETU Nguo zote Ulinipa wewe!!! #MUGACHERERE Nguo zote ulinipa zako… kiukweli Nimepata tabu nyingi Sana Kwenye Mziki wangu Lakini Niliamini Ipo Siku Namimi Nitaonekana.Nashukuru Mungu Sana Kunikutanisha nawewe Brother Naseeb Asante kwa Moyo Wako wa Upendo Kwangu Ulithamini kwa kidogo nilichonacho Nakuamini Nitaweza kufanya.Safari Bado Ndefu Tutafika Tunapotaka!!! @diamondplatnumz
Bongo5