-->

Nisha:Hii Mimba Sio ya Baraka Baraka The Prince

Muigizaji wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’ amedai kuwa endapo ujauzito wake ungekuwa wa Baraka The Prince kama inavyosemwa na wengi basi ungetoka wenyewe mapema kwa kuwa muimbaji huyo ni miongoni mwa wanaume asiowapenda duniani.

nisha-na-baraka-4

Nisha na Baraka enzi za urafiki wao

Akizungumza katika kipindi cha FNL cha EATV, Nisha amesema siri ya mimba yake anayo moyoni na hana haja ya kumtaja mwanaume aliyempatia mimba hiyo.

“Kama hii mimba ingekuwa ya Baraka, ingetoka yenyewe, wala isingesubiri” Alisema Nisha.

Kuhusu muhusika wa ujauzito huo, Nisha ameendelea kufanya siri na kuapa kutomtaja kabisa hata siku moja licha ya watu kutaja baadhi ya majina ya watu maarufu ambao amekanusha kuwa siyo wahusika.

Katika hatua nyingine Nisha aliweka wazi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kiume, licha ya kuwa bado hajamtafutia jina.

Kuhusu mazingira aliyopata ujauzito huo, Nisha ambaye alijikuta akimwaga chozi studio, alisema mwanaume aliyempa ujauzito alimlazimisha kufanya naye mapenzi, na kwamba ahaikuwa ridhaa yake na ndipo ikatokea hivyo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364