-->

Washindi Kutunisha Misuli Kulamba Zaidi ya Mil 17

CHAMA cha Watunisha Misuli Tanzania (TBBF), kimepanga kutoa ajira kwa vijana watakaoshinda kwenye shindano la kutunisha misuli litakalofanyika Desemba 8, mwaka huu.

misubri

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Francis Mafungilo, alisema lengo la kufanya shindano hili ni kusaidia kuwaondoa vijana katika umaskini na makundi maovu.

Mafungilo alisema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atazawadiwa Sh milioni 10, gari, cheti pamoja na medali ya  ushiriki, mshindi wa pili atapata Sh milioni 5, cheti na medali ya ushiriki na mshindi wa tatu atapata Sh milioni 2.5, cheti cha ushiriki pamoja na medali ya ushiriki.

Akizungumza  kwa niaba ya Kampuni ya Pilipili Entertainment Company Ltd, ambayo ni wadhamini wa shindano hilo, msanii Ahmed  Olotu (Mzee Chilo), alisema kampuni hiyo na TBBF imefanya hivyo kwa kuwa imeona umuhimu wa kukuza ajira kwa vijana.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364