Raymond Afunguka Kuhusu Yeye na Alikiba Wakikutana
Msanii wa muziki kutoka label ya WCB, Rayvanny amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na Alikiba ambaye ni mpinzani mkubwa wa boss wake Diamond Platnumz.
Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Salome alioshirikishwa na Diamond, amedai yeye hana tatizo na Alikiba na hata ikitokea nafasi ya kolabo atafanya naye.
“Alikiba huwa nikikutana naye huwa napiga naye stori, tunasalimiana tunacheka, ananiambia kuwa nafanya kazi nzuri, hatujawahi kuongea sana,” Rayvanny alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Aliongeza,”Ikitokea siku naweza kufanya naye kolabo kwasababu ‘end of the day’ wote tunafanya muziki ni biashara pia, mashabiki wetu wanapenda kuona ‘combination’ za watu tofauti tofauti, hata nikikutana naye hatufungiani vioo,”
Diamond na Alikiba wamekuwa wenye bifu kwa muda mrefu huku mashabiki katika mitandao ya kijamii wakidaiwa kulichochea bifu hilo zaidi.