-->

Tamthilia ya Mama Kubwa Mbioni Kukamilika

TAMTHILIA mpya iliyopewa jina la Mama Kubwa inayoandaliwa na Kampuni ya 5 Effects Movies Ltd, ipo mbioni kukamilika baada ya kuandaliwa kwa muda mrefu na kuna uwezekano wa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu.

mtitu

Akizungumza na MTANZANIA jana mmoja wa waandaaji hao ambaye pia ni mmiliki wa kampuni hiyo, William Mtitu, alisema anaamini kazi hiyo itakuwa nzuri kwani waigizaji wamejitahidi kuonyesha uhalisia wakati wa kucheza tamthilia hiyo ambayo itakuwa ni ya kufungia mwaka.

“Tupo katika hatua ya mwisho kuikamilisha tamthilia hiyo tuliyoipa jina la Mama Kubwa ambayo naamini itakuwa katika ubora wa hali ya juu kutokana na wasanii walivyoitendea haki wakati wa kuigiza,” alisema Mtitu.

Aidha, Mtitu alisema kuwa kampuni yake ilisimamisha suala la kutoa filamu na tamthilia kwa lengo la kupisha uchaguzi mkuu uliopita kwani akili za wadau wengi zilielekezwa kwenye kampeni za wagombea wa vyama vya siasa hivyo endapo wangetoa kazi zao wangeingia hasara.

Mtanzania

 

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364