Picha: Harmorapa Amtembelea P-Funk Majani
Msanii mchanga Harmorapa Jumatatu hii alimtembelea producer mkongwe wa Bongo Record, P-Funk Majani nakuzungumza naye mambo kadhaa kuhusu muziki.
Hivi karibuni mtayarishaji huyo mkongwe alionyesha kupendezwa na harakati za rapper huyo ambaye amekuwa akizungumziwa kila kukicha.
Rapper huyo baada ya kutembelea studio hapo na kukutana na mkongwe huyo alionyesha kufurahishwa huku akiwataka watu kuacha kuongea.
“Dreams are brighter days!! Nikiwa na legend producer Majani. Ya leo siyo ya jana hatuongei ongei tu #shout out,” aliandika rapper huyo Instagram.
Kwa upande wa Majani alipost picha aliyopiga na rapper huyo na kuandika :Harmorapa payed us a visit today.