Wema Sepetu Amfungukia Batuli
Ni baada ya Batuli kuongea na waandishi wa habari na kukanusha madai ya kuwa wasanii wa kundi la ‘Mama ongea na mwanao’ lililoshikirika kwenye kampeni za mwaka 2015,wanakidai chama cha mapinduzi.
Kupitia mtandao wa Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya rafiki yake huyo wa zamani na kuandika ujumbe ambao umeashiria kuwa urafiki wao ndio basi tena.
Baada ya ujumbe huo wa Wema, Nay wa Mitego amemchochea muigizaji huyo ambaye wote kwa sasa wanakisupport Chadema kwa kuandika, “✌?️✌?✌?✌? @wemasepetu #MudaWetu Wana Maneno Mengi Tatizo Hawa Action… Usi mwamini ndugu Ata Rafiki, wachukulie Wote wanafiki, ishi tu kivyako Binadamu awa aminiki..! ✌?️✌?.”
Wema Sepetu hivi majuzi akiongea na waandishi wa habari alitoa madai ya kuidai CCM.