Idris Sultan: Mimi na Wema Sio Maadui
Idris Sultan amedai kuwa hana uadui na ex wake Wema Sepetu – bado kwa mbali wana ushkaji.
Mchekeshaji na mtangazaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa huzungumza na ex wake huyo mara chache kwa sasa.
“Unajua sipendi unafiki nikasema ‘ahh tunaongeaga, mbona washkaji tu tuko peace sana’ hapana sio kihivyo,” amesema Idris. “Unakuta ni mara moja moja tu, unakuta hebu leo kuna ka mada fulani mmoja kaamua tu kaposti kitu fulani, mmoja kaamua aamshie humo kwahiyo unakuta na mimi ngoja niongee, kwahiyo sio maaadui, ninachoweza kusema sio maadui.”
Idris na Wema walikuwa na uhusiano maarufu ambao ulikuwa ukivunjika na kurejea tena mara kwa mara.
Bongo5