-->

AT Amtaka Tundaman Kuhamia Kwenye ‘Mauno’

Mfalme wa miduara nchini Tanzania AT ambaye kwa sasa anatamba na ngoma mpya yenye mahadhi tofauti na mduara inayokwenda kwa jina la ‘Sili feel’, amemtaka msanii Tundaman kuanza kucheza ‘mauno’(dansi) ili aweze kupata ‘kiki’ mjini.

Hayo yameibuka baada ya Tundaman kulalamikia vyombo vya habari pamoja na blog kuwapa ‘promo’ nyingi wasanii ambao hawana sifa stahiki huku wenye vipaji kuachwa.

“Kitu cha kwanza inatokana na jambo ambalo lipo wazi, wa muziki wa dansi wenzetu nyimbo zao hawapeleki katika ‘media’ ila zinatafutwa, pia kaka yangu Tundaman wakati alipokuwa anazungumza alisema kuna wasanii wabovu ndiyo wanapata promo lakini angejaribu kuweka sawa, wanaopewa promo siyo wasanii wabovu, aseme madansa ndiyo wanapata promo”– Alisema AT kupitia kipindi cha Enewz kutoka EATV

Msanii huyo aliendelea kumrushia vijembe Tundaman kwa kumwambia kama naye anahitaji ‘promo’ abadili uraia awe mkongo ama atazame njia nyingine ya kutokea nasio kupiga soga tu.

Vile vile amesema ni jambo baya kwa msanii kama yeye kuanza kulalamika ‘promo’ wakati yeye mwenyewe yupo jikoni anapaswa kujipika, huku akimtolea mfano wa mama ntilie anayepika chakula na kupakua chote bila kuambulia hata ukoko.

“Madansa ndiyo wanapata ‘promo’  kwa hiyo kama anaweza kubadili uraia nyimbo zake zikatafutwa sawa, ila kama atashindwa atafute njia nyingine ya kutokea kwasababu hata yeye yupo jikoni, hata ukoko atakosa ?, hii mambo inakuaje si hatari hii”. Alisisitiza AT

Kwa upande mwingine amesema kuna wasanii hawana vipaji ila wanabustiwa na mkwanja ili waonekane wazuri.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364