VIDEO: Kamata, Kafumu Waachia Ngazi
Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya viwanda, biashara na mazingira wamejiuzulu katika nafasi zao kwa madai kamati imekuwa ikikutana na changamoto nyingi zinazowasababishia kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Dalali Kafumu, ambaye ni mbunge wa Igunga na makamu mwenyekiti wake, Vicky Kamata, wametoa taarifa hiyo leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika moja ya kumbi za bunge mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti aliyejiuzulu, Dalali Kafumu, amesema nafasi hizo zimekuwa zikiwafanya kukosa muda wa kufanya majukumu mengine ikiwamo kuwatumikia wananchi hivyo wamepeleka barua ya kujiuzulu kwa spika wa bunge.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti aliyejiuzulu Vicky Kamata amesema kilichomfanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ambazo ameshindwa kuziweka wazi.
Viongozi hao wamezitumikia nafasi hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu huku spika wa bunge, Job Ndugai, akithibitisha kupokea barua ya viongozi hao.
Wasikilize hapa
eatv.tv