-->

Ray Kigosi Amvaa Wema Sepetu Sakata la Roma

Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema tukio la kupotea kwa Roma isiwe sababu ya kutakatisha uchafu wa mtu.

Wema na Ray (2015)

Ray Kigosi ameonyesha kuguswa na kile alichosema Wema Sepetu kuwa baadhi ya wasanii wa filamu wao suala la Roma hawaoni kama linawagusa. Ndipo hapo Ray alipofunguka na kumtaka Wema asiwagombanishe na wananchi.

“Nafikiri ni vema mtu kueleza hisia zake japo sio busara kwa mwenye hisia hizo kuzieleza bila weredi nawasihi wasanii wenzangu kupotea kwa Roma isiwe sabuni ya kutakatisha uchafu wa mtu sote tumesikitishwa na jambo hilo na tumeonyesha kwa vitendo” alisema Ray Kigosi

Ray Kigosi aliendelea kutoa ufafanuzi huku akisema kama Wema anataka kutafuta pointi tatu muhimu katika suala hilo basi amefeli.

“Mimi nimepost inshu ya Roma tangu jana (juzi) usiku Wema sepetu wewe ulikuwa hujapost chochote tuseme ulikuwa huna uchungu? Leo (jana) unaandika kuwa bongo movie hawapo pamoja na tukio la Roma huku ni kutugombanisha na wananchi wanaotuamini. Sisi bongo movie mara nyingi sana tunakuwa pamoja kwenye matukio ya Bongefleva tofauti na wao. Kama una ugonvi na mtu hayo ni mambo yako binafsi ila usitufanye sisi tuonekana wabaya mbele ya jamii utakuwa kichaa kama usipopata maumivu kwa tukio la Roma nimesikitishwa sana post yako Wema Sepetu kama unadhani huu ni muda muafaka wa kutafutia point katika tukio la Roma Mkatoliki umefeli hili ni janga letu sote” alimalizia Ray Kigosi

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364