-->

Jux Afungukia Picha za Vanessa na Wanaume

Msanii Jux ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Umenikamata’ amefungaka na kusema kitendo cha Vanessa Mdee kuonekana akipiga picha na wasanii mbalimbali au wanaume hakimpi shida kwani yeye anaamini zile ni kazi.

Jux na Vanessa

Jux anasema yeye aliamua kutoweka wazi mambo yake na Vanessa kutokana na ukweli kwamba ilifika wakati watu walikuwa hawazungumzii kazi zao zaidi wanazungumzia mambo yao ya mahusiano hivyo waliamua kuweka pembeni mambo hayo ili watu wawezi kufuatilia kazi zao, ila si kweli kwamba yeye alivimba baada ya kuona Vanessa akipiga picha na wasanii kama Ice Prince Zamani, Trey Songz,

Kwanza si kweli mimi nilimaidi, sababu kama kupiga picha za namna hizo Vanessa anapiga na watu wengi sana picha za namna ile ila naomba nirudi nyuma kusema hili tena wasichana kwenye tasnia yetu sisi wavulana ndiyo tunatakiwa kuwasapoti sana sababu wapo wachache, na wengi huwa wanakata tamaa kwa vitu kama hivi. Vinaweza kuwa ni vitu vya kawaida katika mapenzi vipo lakini haviwezi kufika hatua hiyo sababu mimi najua ile ni kazi. Kwa hiyo mimi nikionyesha kuwa nimemaindi Ice Prince kupiga picha zile na V sidhani kama ni sawa, sababu mimi mwenyewe kwenye video zangu nawabeba watoto, nawashika, nalala nao vitandani lakini mwisho wa siku najua ile ni kazi kwa hiyo ile siyo sababu” alisisitiza Jux

Mbali na hilo Jux anasema ni kawaida wao kupishana katika vitu vidogo ila haijawahi kutokea yeye akafanya vitu ambavyo vinaweza kumrudisha nyuma Vanessa Mdee katika kazi yake ya muziki.

“Kuna vitu vya kawaida sisi ni binadamu tunapishana lakini siyo vitu vya kusema mimi ni maindi, kwa hiyo hata siku moja katika kazi za V sijawahi kuonyesha hata kitu kimoja cha kumrudisha nyuma, mimi hata nikipiga picha na wanawake kumi hapa watu watajua tu Jux anafanya video ila Vanessa akipiga picha hizo watu watasema huyu mwanamke muhuni kwa hiyo wanawakati mgumu sisi wanaume tunapaswa kuwatete mabinti hawa maana wapo wachache kwenye muziki” alisisitiza Jux

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364