-->

VIDEO: Chadema awana Shukrani – Wolper

Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka sababu za kuacha kuendelea kuisapoti CHADEMA ni viongozi wa chama hicho kushindwa kuutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi mkuu hali iliyomfanya ajihihisi mpweke na kama ametelekezwa .

kiwa ni mara ya kwanza Wolper kufunguka ishu hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV, amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata shilingi elfu 10 za kitanzania.

Pamoja na kuwa alifanya kampeni za kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364