-->

Video : Q Chief Amtabiria Mazito Chid Benz

Msanii Q Chief amefunguka kwa kudai ameamua kumrudisha tena mkali wa ‘free style’ Chid Benz katika ulimwengu wa muziki.

Q Chief amebainisha hayo baada ya kusambaa picha mtandaoni zilizokuwa zinawaonyesha wawili hao wakiwa studio ambapo watu wengi walianza kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu ndani yake.

“Chid Benz ni moja kati ya ma-rapa ambao wanahistoria kubwa sana katika ukanda huu wa East Afrika, pia unapomzungumzia Chid Benz unamzungumzia moja kati ya rapa ambao wana tuzo zaidi ya tatu au nne za Hip hop na ‘so far’ nikijaribu kuangalia kwa Tanzania nani amechukua tuzo tatu, nne nawaona Weusi” alisema Q Chief

Pamoja na hayo, Q chief amesema maisha aliyopitia swahiba wake Chid Benz hata yeye ameyapitia hivyo hajisiki vizuri kuona anamuacha bila ya kumsaidia kwa namna moja ama nyingine.

“Rashid ni rapa mzuri amepitia kwenye ‘situation’ ambazo hata mimi niliwahi kupitia. Nilishawahi kuhojiwa na mtandao mmoja mkubwa Tanzania nikaulizwa unadhani nini kifanyike kwa Rashidi, kikubwa nilichokisema ndicho kilichofanyika, nilisema kwamba dawa ya Rashid anayo yeye mwenyewe hatuna sisi, yeye mwenyewe ana tiba yake na tiba ni kukubaliana na nafsi yako kwamba upo kwenye giza unahitaji kwenda kwenye nuru. Nilichokifanya mimi ni kumkoseza Rashidi karibu na Mwenyezi Mungu kwa sababu tunaishi lazima ujue kuna Mungu” aliongezea Q chief

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364