-->

Wema Sepetu na Gabo Zigamba Ndani ya KISOGO (Video)

Malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu, ameweka bayana ujio wa filamu fupi mpya ya “Kisogo” aliyofanya pamoja na muigizaji mwenzake Gabo Zigamba, itakayo weza kupatikana kwa njia ya mtandao.

Wema amebainisha hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka kionjo cha filamu hiyo pamoja na ujumbe huu.

“Asikwambie Mtu Kuigiza Raha bwaaana… Sema ndo uwe unajua sasa…. Sio tu unaigiza ili mradi…. Afu pia ujue kuitendea haki character yako… Maana ukishakaa mbele ya Camera unasahau kabisa kama wewe ni Wema Sepetu sijui Tz Sweetheart… Unaweka pembeni na unavaa uhusika wako unaotakiwa…. Sidhani kama nimewahi kuwaangusha… Tanzama best short Film kiganjani kwa kutumia simu popote ulipo kutana na @gabozigamba1@wemasepetu @millardyayo ndani ya #kisogo
Dondosha App ya Uhondo tv bureee. Mwaka Huu Mbona Kama Kuna Raha Nyingi.” aliandika Instagram.

Wawili hao kwa sasa wanafanya kazi kwa ubaribu zaidi baada ya miezi kadhaa iliyopita kuweka wazi ujio wa filamu yao ya pamoja itwaayo, ‘Heaven Sent’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364