Snura na Ben Pol Eti Wanazingua!
WANAZINGUA. Hayo ni maneno ya mashabiki wakiwatupia wasanii Snura Mushi ‘Chura’ na Ben Pol baada ya wasanii hao kujibizana wenyewe kwa wenyewe kwenye vyombo vya habari na kugeukana.
Snura na Ben Pol, katika Usiku wa Fiesta Dodoma mwishoni mwa mwaka jana, wakati wanatoa burudani walionekana wakikumbatiana kimahaba huku wakipeana mabusu moto moto jukwaani na kusababisha mashabiki kulipuka kwa shangwe huku wengine kudai ni wapenzi.
Katika kuthibitisha hilo, baada ya kitendo hicho kudumu kwa dakika tatu, Ben Pol akamtambulisha Snura kuwa ni mpenzi wake.
Hata hivyo, hiyo yote ilikuwa ni mipango ya kiongozi wao aliyewataka wafanye hivyo ili kuchangamsha mashabiki kutokana na ratiba kwani ilitakiwa Ben aanze kupanda jukwaani kisha Snura afuate na aitwe kwa staili hiyo.
Sasa mizinguo inakujaje? Wiki hii hali imekuwa mbaya kwa wawili hao baada ya kusutana hadharani katika chombo kimoja cha habari kuwa baada ya tukio lile mmoja wao akatangaza kwa watu kuwa alikuwa siriazi kwa kumtaka mwenzie.
Snura amemshutumu Ben Pol kuwa amemtangazia alikuwa anamtaka kimapenzi kabla ya Ben kukanusha hapo hapo na kudai hakusema chochote, ndipo mashabiki wakasema wanazingua na kutafuta kiki ili waweze kutoa wimbo au ni wapenzi ambao wameshaachana huku wakipendana. Huu ndiyo ubuyu wa mjini.
Mwanaspoti