-->

Ebitoke: Ben Pol Akinikataa, Usichana Wangu Nitampa Atakayenioa

TASNIA ya ucheshi nchini imekuwa na idadi ndogo ya wachekeshaji wa kike, hali kadharika wa kiume wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa zinazopeleka sanaa yao kutotiliwa uzito mkubwa licha ya umuhimu wake, angalau kwa sasa tunaweza kuona wachekeshaji wa kisasa wakiingiza fedha ndefu.

Wiki za hivi karibuni mchekeshaji wa kike, Ebitoke amekuwa kwenye vinywa vya wapenda burudani wengi hiyo imetokana na kufanya sanaa yake kwa ubunifu wa hali ya juu kiasi cha kuwalizimu mashabiki kumfuatilia.

Ni Exclusive, Juma3tata leo tupo na mrembo huyu ambaye amejidhatiti kuhakikisha maisha yake yote anaitendea haki sanaa ya uchekeshaji na kuweka alama ambayo haitafutika hata pale atakapokuwa hayupo duniani, karibu.

Juma3tata: Wadau wa ucheshi nchini wanapenda kumfahamu Ebitoke ni nani haswa?

Ebitoke: Naitwa Anna Exavery maarufu kama Ebitoke, nimezaliwa huko Bukoba lakini mimi ni Mkerewe, kwenye familia tupo watoto 11 na mimi ni mtoto wa 10 kuzaliwa.

Juma3tata: Safari yako ilikuwaje mpaka ukaingia kwenye sanaa?

Ebitoke: Kiukweli mimi sanaa ilikuwa ‘passion’ yangu, na rasmi nilianza mwaka jana mwishoni, nilitafuta nafasi ya kufanyia sanaa yangu, bahati nzuri nikaona tangazo la Timamu African Media watafuta wasanii na mimi nikajitokeza kwenye usahili Mungu akanisaidia nikapita, nilikuwa nafanya filamu za kawaida lakini ‘director’ wangu aligundua kuwa nina kitu cha ziada akanishauri kwanini nisifanye komedi, ndiyo hapo nilipoanza uchekeshaji.

Juma3tata: Mawazo ya vichekesho vyako huwa unavitoa wapi?

Ebitoke: Sisi kama Timamu Comedians tupo kama timu ambapo huwa tunakaa tunaanza kujadili ‘idea’, lakini sana sana Idea nyingi huwa zinatoka kwa meneja wetu.

Juma3tata: Mchekeshaji gani wa kike Afrika Mashariki anakuvutia?

Ebitoke: Hakuna msanii wa kike wa komedi anayenivutia, sioni najiona mimi tu peke yake.

Juma3tata: Umetangaza kuwa unampenda staa wa muziki wa RnB, Banard Paulo ‘Ben Pol’, je ukimtazama sehemu gani ya mwili wake inakuvutia zaidi?

Ebitoke: Kiukweli mimi nampenda sana Ben Pol sana tena sana na ninatamani anioe kabisa, lakini sasa kuhusu masuala ya sehemu ipi inanivutia siwezi kujibu sababu vingine natakiwa kuvijua mimi tu na siyo watu wengine.

Juma3tata: Ikitokea amekataa kukuoa utafanya maamuzi gani hasa ukizingatia umesema umemtunzia usichana wako?

Ebitoke: Napenda watu waelewe kitu kimoja, mimi sijampenda Ben Pol kisa nimpe bikra yangu, kwa mfano akikataa kunioa basi nitamwacha aendelee na familia yake, kwa sababu watu wanaongea kinoma, lakini kuhusu hilo nitaendelea kujituza mpaka mwanaume wa kweli atokee kwenye maisha yangu ndiyo nitampa bikra yangu.

Juma3tata: Unazungumzia suala la Ben Pol kutumia kiki kwenye muziki wake?

Ebitoke: Kuhusu kiki kwenye muziki wake kwa kweli hivyo mimi havinihusu, hivyo vyote ni sehemu ya kazi yake kwa sababu mimi ninachohitaji kwa Ben Pol ni upendo tu basi, hayo mambo ya kiki aendelee tu kwa kuwa kila mtu ana mipango yake kwenye maisha.

Juma3tata: Changamoto gani unakutana nazo kwenye sanaa yako ya uchekeshaji?

Ebitoke: Kwa upande wangu naweza kusema changamoto ni kazi yangu ambapo inanilazimu kila siku niumize kichwa ili kupata ‘clip’ mpya kwa sababu vichekesho vyetu vipo tofauti na wengine mambo mengine ya kawaida tu hakuna changamoto kubwa.

Juma3tata: Mipango yako ni ipi kuhakikisa sanaa yako inavuka boda?

Ebitoke:  Mipango ipo na ninaweza kusema katika kampuni yetu tumeshaanza kufanya kazi ambazo zinaenda kuwa kimataifa zaidi, lengo ni kuhakikisha sanaa inaenda mbele ili na sisi tuzidi kupata manufaa kwa nchi yetu.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364