Kwa Nini Wolper Hakumfariji Zari Alipofiwa na Mmewe? Majibu Yapo Hapa
KUFUATIA wadau mbalimbali kumtuhumu kwamba, hana utu kwa kushindwa kwenda kumfariji rafiki yake, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ hivi karibuni alipofiwa na mzazi mwenzake, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ huko Uganda, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibuka na kufungukia sababu za kutofanya hivyo.
Akizungumza na Wikienda, Wolper alisema kuwa, ulipotokea msiba wa Ivan, yeye alikuwa nchini Burundi alikokwenda kwa ajili ya kuchukua mzigo wa dukani kwake hivyo alikuwa bize na hata kama angekuwepo Bongo asingeweza kwenda kwani Zari siyo rafiki yake wa kihivyo.
“Nilikuwa bize na biashara na hata kama isingekuwa hivyo nisingeenda kwa sababu sina ukaribu wa kihivyo na Zari bali siku zile kwenye video iliyosambaa nilikuwa namtetea kwa sababu sipendi mtu aonewe, yaani watu wanamweka mitandaoni amezeeka wakati ukimuona live ni mzuri na mrembo kabisa, sipendi uonevu katika maisha yangu, mimi ni mtetezi wa wanyonge, sema watu hawanijui wananichukuliaga tofauti,” alisema Wolper.
Stori: Gladness Mallya, Dar/ GPL