-->

Mama Mzazi wa Zari, Afariki Dunia!

Mama mzazi wa Zari The Boss Lady ambaye ni mpenzi na mzazi mwenza wa mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz amefariki dunia asubuhi ya leo hii baada ya kuumwa.

Kupitia Instagram yake asubuhi hii Zari amethibitisha kifo cha mama yake akiandika>>>”Kwa huzuni kubwa mimi na familia yangu tunatangaza kifo cha mama yetu mpendwa aliyefariki asubuhi hii. Roho yake ilazwe pema, Allah akisamehe dhambi zako na akujaaliye Jana. Tutakupenda zaidi, sisi kama watoto wako tulipewa kilicho bora kutoka kwa Mungu kama mama yetu. Tunathamini yote uliyotenda kwetu. Tutakuthamini daima Mama. Lala salama

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.

Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga, aliyeaga dunia Mei 25 mwaka huu huko Steve Biko Academic Hospital nchini Pretoria, Afrika Kusini.

Pumzika kwa Amani, Halima Hassan.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Hi there!

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364