-->

Baada ya Kumuita Nyani, Iyobo Amvaa Tena Harmorapa

KIONGOZI wa madansa ambaye ni dansa tegemezi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Mose Iyobo amefunguka kuwa yeye hana imani na Harmorapa na anashangaa anavyotajwa kila mahali kwani yeye hajawahi kusikia kazi yake yoyote hivyo hajui uwezo wake kimuziki.

Iyobo aliendelea kwa kutoa povu kuwa yeye anamchukulia Harmorapa kama mtu aliyekurupuka kwenye muziki na hajui ni nini anachotakiwa kufanya.

Kupitia eNewz ya EATV Iyobo alifunguka hayo huku akikazia kuwa muziki si jambo la mchezo mchezo bali unahitaji kujipanga.

 

“Mimi ni mtu ambaye nipo kwenye muziki muda mrefu, kila siku nyimbo mpya zinapotoka ziwe za watu maarufu hata wasio maarufu nazisikia lakini mimi sijawahi kusikia kazi yoyote ya Harmorapa, kwa hiyo sina cha kumshauri ila hiyo kazi anayofanya inahitaji mtu makini, anayekwenda na wakati na siyo kukurupuka tu na kufanya ghafla sababu hiyo kazi ina pesa nyingi na inatia umasikini kwa haraka sana kama hufanyi vile inavyotakiwa,” alisema Mose Iyobo

Salum Milongo/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364