Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Abby Skills amemchana msanii mwezake Hakeem 5 kutuliza akili yake na arudi kwa Ally Kiba amuombe msamaha kwa kuwa Kiba hana tatizo na mtu.
Akiongea ndani ya eNewz, Abby amesema Hakeem 5 alimkosea sana Alikiba na kumshauri arudi nyuma na kuomba msamaha kwa kuwa mwanamuziki huyo hana kinyongo na mtu yeyote.
Pia Abby amesema Ally ni mtu wa watu ni mkarimu na hana ugomvi na mtu yeyote hivyo Hakeem 5 asimuongelee vibaya kwa kuwa Kiba anamsikiliza kila mtu hivyo atulize kichwa chake.
eatv.tv
Comments
comments