Mwanamziki wa bongo fleva kutokea king music, Abdukiba amekanusha vikali kutoka kimapenzi na mpenzi wa mwanamziki mwenzie Rayvanny aitwae Fayvanny.
Mwanamziki wa bongo fleva Abdu kiba pia ni maarufu sana kwa sababu ya undugu alionao na staa wa bongo fleva Alikiba, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na iliyomuonesha yeye na mke wake wa Rayvanny.
Kipindi cha nyuma kidogo kuna video ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonesha abdukiba na baby mama wa Rayvanny anaye julikana kama Fayvanny wakiwa wamepozi wanapiga stori
Inajulikana wazi kuwa Rayvanny yupo WCB na Diamond ni bossi wake lakini pia inajulikana kuwa Diamond na Alikiba ni paka na panya hivyo hiyo inapeleka makundi haya kuwa na bifu.
Baada ya sakata hiyo Abdu kiba kwenye interview aliofanya millardayo tv ambapo amedai kuwa amemjua fayvanny tangu zami sana na ile video ni ya kitambo kipindi hicho fayvanny alikuwa mshabiki wake.
“Nilimjua yule msichana tangu alivyokuwa anafanya kazi kule Tv ONE na tulikuwepo tunafanya interview ya television na kati kati ya interview tukarekodi ile video na kipindi kile alikuwa shabiki wangu mkubwa lakini hiyo ilikuwa zamani kabla hawajawa na Rayvanny nahisi tangu amekuwa kwenye mahusiano na Rayvanny sijawasiliana naye”- ABDUKIBA
Comments
comments