BAADA ya kutangaza kuachana na siasa, mwanamuziki wa Hip Hop, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na kuwaomba msamaha mashabiki zake aliowakwaza kipindi yuko kwenye siasa na sasa alivyojiondoa.
Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi, Afande Sele alisema anawaomba msamaha wote kutokana na kuingia na kutoka kwenye siasa hivyo wamuunge mkono kwenye muziki kwani amerudi rasmi.
“Nawaomba mashabiki zangu wanisamehe, wanipokee kwa mara nyingine kwenye muziki kwani nakuja na kazi mpya nzuri, nguvu zote nimezielekeza kwenye muziki sasa,” alisema Afande Sele.
Hivi karibuni Afande Sele ambaye alikuwa ni mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo pia aligombea ubunge kwenye uchaguzi uliopita, alitangaza kuachana na siasa na kurudi rasmi kwenye muziki.
Chanzo:GPL
Comments
comments