Album ya Diamond Kupatikana Duniani Kote
Msanii Diamond Plutnumz ambaye yuko kwenye mikakati ya kutoa albam yake itakayouzwa kimataifa, ameweka wazi mikakati yake ya kuisambaza album hiyo, ili iweze kupatikana duniani kote.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema mwanzo alikuwa hajafanikiwa kutoa albam kwani alikuwa anaangalia soko jinsi lilivyo, na aljikita zaidi kwenye mitandao ili kujitambulisha zaidi, lakini sasa yupo tayari kwa soko la albam kimataifa.
Diamond aliendelea kusema kwamba sababu nyingine ya kuita albam hiyo ya kimataifa ni kwa kuwa anapanga kuchanganya muzii wenye ladha tofauti tofauti, zikiwemo za Tanzania na nje ya Tanzania, na atahakikisha albam hiyo inapatikana duniani kote.
“Ninaposema Internationa album simaanishi kwamba haitauzwa tanzani, itauzwa Tanzania kwanza, lakini itaweza kufika ulimwengu mzima, naweka ladha tofauti tofauti, za kitanzania na zilizoko nje ya Tanzania, nilikwama kutoa album hapa kati kwa sababu ya kuangalia hata soko la kitanzania lilivyo, ilibidi nijidhatiti katika suala la kidigitali kwa sababu ndo mauzo mengi yanatokea humo, nafanya nyimbo ambazo nikipeleka kwa watu ni rahisi wao kuzipenda kama Amerika, nchi nyingine za Afrika, so nitahakikisha kila nchi ulimwenguni inapatikana”, alisema Diamond.
Albam hiyo itakuwa ni album ya tatu kwa msanii huyo, lakini itakuwa ni albam ya kwanza kwake ya kimataifa.
eatv.tv