Mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii mkongwe wa bongo fleva Prof Jay, kwa Mara ya kwanza ametoa ya moyoni baada ya nyumba yake kubomolewa na TANROADS.
wenye ukurasa wake wa instagram Prof Jay ameandika ujumbe akisema amejifunza kumshukuru Mungu, huku akuonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kutoheshimu uamuzi wa mahakama kama mhimili wa nchi.
“Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , limenisikitisha zaidi”, ameandika Prof. Jay.
Prof. Jay ameendelea kuandika akisema …”Nimejifunza kumtegemea na kumshukuru Mungu kwa kila jambo, na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na naamini tutashinda”.
Kwa mujibu wa Prof Jay nyumba yake imebomolewa Septemba 29,2017, na hakufanikiwa kuokoa kitu chochote ambacho kilikuwemo.
Comments
comments