Alikiba Afunguka ‘Kummiss’ Dada yake Diamond
Msanii wa bongo fleva Alikiba amefunguka na kusema kuwa kuna wakati huwa anamkumbuka sana msanii wa kike ambaye ni dada wa msanii Diamond Platnumz Queen Darleen.
Ikumbukwe kuwa msanii Alikiba kipindi cha nyuma aliwahi kufanya kazi na msanii Queen Darleen na walikuwa na ukaribu wa hali ya juu kiasi kwamba wapo watu walihisi kuwa labda ni wapenzi.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kwenye heshima ya bongo fleva wiki kadhaa zilizopita ambapo Alikiba alikuwa mgeni rasmi alifunguka na kusema yeye mwenyewe anamkumbuka Queen Darleen sababu kuna vitu walikuwa wanaendana.
“Queen Darleen alikuwa mkongwe katika gemu na tulikuwa na ukaribu sana. Kiukweli muda mwingi huwa nina ‘M-miss’ sababu mimi na yeye kuna vitu vingi tulikuwa tukiendana kama washikaji. Muda mwingine akili yangu na yake ni kama sawa vile” Alisisitiza Alikiba
Mbali na hilo Alikiba alifunguka na kusema Producer wake wa zamani KGT amemtumia beat ambayo yeye mwenyewe amekiri kuwa ni biti nzuri inayompa hisia kali sana anapoisikiliza na kudai kilichobaki ni kwenda kukutana na KGT na kufanya kazi hiyo.
“KGT amenitayarishia mkono mmoja mzuri sana kila naposikiliza beat ile natamani kulia. Ile biti natakiwa nikaingize sauti na kufanya kazi mpya na KGT kwani kwa muda mrefu sasa sijakutana naye live” alisema Alikiba
eatv.tv