Alikiba Afungukia Ujio wa Ngoma Mpya
Msanii Alikiba ameweka wazi mipango ya mkongwe wa muziki Abby Skillz, kuwa muda si mrefu atakuja na ngoma yake mpya baada ya ngoma yake ya ‘Averina’ ambayo alikuwa ameshirikishwa yeye pamoja na Mr Blue ambayo ilitoka mwaka jana.
Abby Skillz ni kati ya wasanii ambao walidaiwa kuwa chini ya usimamizi wa Alikiba kupitia ‘Label’ yake ya King’s Music ambapo Alikiba aliwahi kusema kuwa baada ya kuachia wimbo wake mpya ambao ni ‘Seduce Me’ alisema baada ya hapo utakuwa ni wakati wa wasanii waliopo kwenye Label yake hiyo kutoka na ngoma zao pia.