Mastaa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Alikiba na Diamond Platnumz wametajwa kwenye orodha ya vijana 100 waliochini ya miaka 40 wenye ushawishi zaidi barani Africa kwa mwaka 2017.
Kwenye orodha hiyo iliyotolewa leo na mtandao wa African Youth Awards imemtaja pia muigizaji wa filamu nchini Tanzania mrembo Elizabeth ‘Lulu’ Michael na mwanamitindo Flaviana Matata na mwana habari maarufu Millard Ayo kwenye orodha hiyo ya vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Africa.
Kwa upande mwingine wasanii waliochaguliwa kwenye orodha hiyo kutoka nje ya Tanzania ni Davido kutoka Nigeria , Rapa AKA kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.
Dirisha la kupendekeza majina ya vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika mwaka 2017 lilifunguliwa mwezi June 25 na kufungwa agosti 22 mwaka huu.
Comments
comments