Mfalme wa bongo fleva Alikiba mwaka huu ameamua kuzunguka duniani kukutana na mashabiki wake na kutanua wigo wa muziki, mwezi Julai anatarajia kuanza ziara yake katika bara la Ulaya ambapo ‘show’ ya kwanza ataipiga na mkali kutoka Nigeria Davido.
Katika ‘show’ hiyo ambayo itawakutanisha Alikiba na Davido itafanyika Ubelgiji na baada ya hapo mkali huyo wa Aje ataendelea na ziara yake hiyo ya kukutana na mashabiki zake ili kuzidi kutanua wigo wa muziki wake kimataifa.
Meneja wa Alikiba Bi. Seven Mosha amethibitisha wakali hao kukutana katika ‘show, mwezi wa saba huku akisema kuwa ziara hiyo ya Alikiba imekuwa na matokeo chanya kwa msanii huyo pamoja na muziki wake, huku akidai kwamba ziara hiyo itaendelea kufanyika katika miji mingine mbalimbali.
EATV.TV
Comments
comments