STAA wa Series Comedy kali ya Side wa Kitonga Said Bakary Mbelemba aka Side Jangala Junior inayotamba katika Luninga ya E Tv amefurahishwa sana na kukubalika January Makamba-Waziri wa Nchi, Ofisi ya M/Rais, Muungano na Mazingira kupitia Side wa Kitonga ambayo inakimbiza kupitia kituo chako cha Luninga cha E Tv.
“Unajua unakutana na mtu mkubwa na waziri mwenye dhamana kama Mh. Makamba na anakukubali kazi yako ni faraja kubwa sana kwangu na inanipa nguvu na deni kuhakikisha simwangushi,”alisema Side wa Kitonga.
Side anafanikisha kuwapatia burudani wapenzi wa Comedy Bongo akiwa na rafiki yake wa karibu Kalombo Amboni, mwanadada Naomi Chuwa wakiwa kazini vijna hawa ni hatari sana katika kuhakikisha wanakupa Elimu na Burudanihili ni chimbuko la Tanzania Movie Talent.
Side wa Kitonga uruka kila siku ya Alhamisi saa 3:00 Usiku na kurudi siku ya Jumamosi saa 6:00 mchana, jumapili, Jumatatu 5:00 Usiku na siku ya Jumatano saa 5:00 Usiku ni kazi inayoandaliwa na kampuni ya Production X ya jijini Dar Es Salaam wataalamu wa utengenezaji wa Filamu, vipindi makala (Documentray) na Production kwa ujumla.
Filamu Central
Comments
comments